Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Serikali ya kaunti ya Nakuru imesema kwamba itawachukulia hatua kali za kisheria wazazi, walezi ambao wanawanyima watoto haki ya kupata elimu.

Katibu wa kaunti ya Nakuru Joseph Motari alikiri kuwa ni kinyume cha sheria kwa mtoto anayefaa kuwa shuleni kunyimwa haki ya kupata elimu, ilhali kuna serikali inayozingatia elimu ya watoto.

Aidha Motari amesema kuwa serikali ya gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua imekuwa kitoa kipaumbele kwa maswala ya elimu.

Kwa muda wa siku tatu zilizopita ametumia milioni mbili kwa ajili ya kugaramia masomo ya watoto mayatima na wasiojiweza katika kaunti ya Nakuru.

Matamshi hayo yanajiri majuma matatu baada ya gavana Kinuthia Mbugua kupeana basari ya zaidi ya shilingi milioni hamsini na tano ili kufadhili elimu ya wanafunzi waliyopita na wasiyo na uwezo wa kumudu karo.