Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wazazi katika Shule ya msingi ya Nyakemincha katika eneo bunge la Mugirango Magharibi, Kaunti ya Nyamira, wamelazimika kuwaondoa watoto wao katika shule hiyo kufuatia ukosefu wa walimu.

Hii ni baada ya walimu tisa waliokuwa katika shule hiyo hapo mbeleni kupewa uhamisho hadi shule zingine tofauti.

Walimu waliopata barua za kuenda kufundisha katika shule hiyo walisusia agizo hilo, huku wanafunzi wakiachwa bila walimu.

Akihutubia waandishi wa habari siku ya Jumatano shuleni humo, mkuu wa elimu katika Kaunti ya Nyamira Titus Mbata alisema atajaribu kila awezalo kuhakikisha kuwa wanawaajiri walimu watakaofunza katika shule hiyo.

Wazazi wa shule hiyo, wakiongozwa na James Bosire, walikosoa usimamizi wa shule hiyo huku wakiapa kutowarudisha watoto wao katika shule hiyo.

Wazazi hao walisema kuwa walimu waliopewa uhamisho kwa shule hiyo walisusia agizo hilo, kufuatiashule hiyo kuandikisha matokeo duni.

“Walimu waliokuwa katika shule hii walihamishwa kwingine na watoto wetu wamekuwa wakivumilia huku wakilazimika kujifunza,” alisema James Bosire

Aliongeza, “Hatutakubali watoto wetu kuendelea kuteseka na tumeapa kutowarudisha katika shule hiyo.”