Wazee wa Nyumba Kumi katika eneo la Moricho, kaunti ndogo ya Rongai wanadai maisha yao yamo hatarini baada ya zaidi ya wapishi 70 kutoka eneo la Legitio kutishiwa maisha yao.
Wapishi wa pombe haramu walivamia eneo la Moricho Jumapili saa moja jioni huku wakiwa wamejihami kwa silaha ikiwemo mapanga na mishale wakitishia kuwakatakata wazee hao.
“Kama si mke wangu ningekuwa nimeangamizwa, hao watu walikuwa tayari kutekeleza waliyokuwa wakikusudia,” alisema Kiprono.
Naye Harun Chebii alisema kuwa, anahofia maisha yake na familia yake kwani hajui watakaporejea watu hao.
“Sasa tunahofia maisha yetu maanake hao watu wakati wowote wanaweza kutuvamia, tunaomba serikali ituimarishie usalama wetu," Kiprono alisema.
DC Wa Rongai David Koskei na OCPD Wa Rongai Joseph Mwamburi waliwatuma maafisa wa polisi ili kuhakikisha kwamba, hali ya utulivu imerejea katika eneo hilo.