Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wenyeji wa eneo bunge la Mugirango Kusini kaunti ya Kisii ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakingoja habari njema kuhusu ujenzi wa kiwanda cha kusaga sukari katika eneo lao wamepongeza kaunti kwa kusema kuwa ujenzi huo utawanufaisha wakazi hao.

Akiongea wakati wa sherehe za usinduzi wa soko la Riosiri, mapema wiki hiii Gavana Ongwae alisema kwamba serikali yake imepiga hatua mathubuti katika mipango hiyo na kuongeza kusema kuwa tayari ardhi ambayo kiwanda hicho kitajengwa imepatikana.

Kwa muda mrefu, wenyeji wa eneo hilo la Mugirango Kusini ambao wengi wao ni wakulima wa miwa wamekuwa wakiteseka na mazao yao kwasababu ya uchache wa viwanda hivyo vya kusaga sukari hivyo basi ujenzi wa kiwanda kitawaletea afueni.

Kwa upande wa maji ambayo ni adimu sana katika eneo hilo, Gavana James Ongwae alisema kwamba serikali yake itakarabati mradi wa Mosache na kusambaza maji katika eneo hilo hasa katika soko la kisasa la Riosiri ambalo lilizinduliwa mapema wiki hii.