Afisa mkuu mtendaji wa mahakama ya Mombasa Zakayo Otieno alifika kizimbani kujibu maswali ya kwa nini mahakama inajikokota kutafuta mkalimani wa lugha ya kifarsi.
Mkalimani huyo anahitajika katika kesi inayomkabili mwana wa Ibrahim Akasha na wenziwe.
Zakayo aliiambia mahakama kuwa anapata changamoto ya kupata mkalimani huyo katika eneo la Pwani, na kuihakikishia mahakama kuwa anashirikiana na wenzake kumtafuta mkalimanai huyo.
Hii ni baada ya naibu mkurugenzi mkuu wa mashataka ya umma Alexendra Muteti kuiambia mahakama kesi hiyo imekwama kwa sababu ya kizingiti cha lugha.
Mmoja wa washtakiwa hao Gulam Hussein haelewi lugha ya kiingereza inayotumiwa kwenye vikao vya kesi hiyo.
Washtakiwa hao wanahitajika na serikali ya Marekani kufunguliwa mashtaka hayo.
Kesi hiyo itatajwa Novemba 12 kubaini iwapo mkalimani huyo amepatikana.