Share news tips with us here at Hivisasa

Seneta wa kaunti ya Nyamira Kennedy Okong’o amevishauri vikundi vya akina mama kuweka pesa zao katika benki kama njia moja ya kuzuia visa vya kuibiwa na washukiwa wa ujambazi.

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa mara nyingi majambazi huvishambulia vikundi vya akina mama wakati wamekusanya pesa.

Seneta okong’o alwashauriwa akina mama kutekeleza shughuli hizo za kusanya pesa wakati benki zimefunguliwa.

Akizungumza siku ya Jumapili mjini Nyamira, Okong’o alisema njia moja ya kupunguza wizi wa aina hiyo ni kuweka pesa wanazozikusanya kwa benki kila wakati.

Katika siku za hivi maajuzi, majambazi katika kaunti ya Nyamira wamekuwa wakiwaangaisha wakazi kwa kuwashambulia na kuwanyanganya pesa na bidhaa vingine.

“Naomba akina mama wakati mnakusanya pesa za vyama au vikundi mnahakikisha kuwa benki zimefunguliwa ili muweka pesa hizo huko siku hiyo hiyo. Msiruhusu yeyote kuenda na pesa hizo kwake maana majambazi wamekuwa wakiwasumbua sana hapa Nyamira,” alisema Okong’o.

Wiki jana kamishna wa Kaunti ya Nyamira Josephine Onunga aliomba wakuu wa polisi katika kaunti ya Nyamira kuimarisha usalama katika kaunti hiyo.