Share news tips with us here at Hivisasa

Balozi wa umoja wa mataifa al maarufu United Nations Habitat Profesa Sam Ongeri amewaomba wananchi kuheshimu viongozi waliochaguliwa ili kufanyiwa maendeleo zaidi.

Akizungumza mnamo siku ya Jumapili katika Kanisa ya Kiadventista ya Valley iliyoko eneo Bunge la Borabu katika Kaunti ya Nyamira, profesa Ongeri aliwaomba wananchi kuwaheshimu viongozi walio mamlakani na kuwa na umoja ili kuhakikisha maendeleo yamefanyika kikamilifu.

Aidha, Ongeri aliwaomba wazazi wote katika eneo la Gusii kuwafundisha wanao tabia ilioyo njema wangali wachanga ili wanapokuwa watu wazima wawe na tabia nzuri ya kufurahisha katika jamii.

“Naomba wazazi wote kuwasomesha watoto ili waje kujisaidia nyakati zijazo maana masomo ndio nguzo ya maisha na muwe mnawaonyesha tabia ya kuwa na heshima kwa watu katika jamii,” alisema profesa Ongeri, balozi wa umoja wa mataifa.

Pia Ongeri aliwaomba viongozi wote waliochaguliwa kuhakikisha kuna amani sehemu wanazoziongoza na kuwa na umoja na kufanya maendeleo kwa wananchi waliowachagua.

“Viongozi waliochaguliwa wafanye maendeleo na wawe na umoja pamoja na kuhubiri amani miongoni mwao ili nchi ya Kenya iweze kusonga mbele kimaendeleo,” aliongeza Ongeri.

Ongeri alisisitiza kuwa, “Zile nchi zingine ambazo viongozi wana umoja zimeendelea mbele na nchi zile hazina umoja, mandeleo yamerudi nyuma. Sisi Wakenya tunahitaji nchi yetu isonge mbele kimandeleo na tuwe na umoja miongoni mwetu ili kuwafurahisha wananchi wa Kenya kimaendeleo.”

Matamshi ya balozi huyo yaliungwa mkono na Waziri wa Mawasiliano nchini Fred Matiang'i aliyewaomba wananchi na viongozi kuwa na umoja na kuhubiri amani nchini Kenya.