Wakazi wa Manga wana kila sababu ya kutabasamu baada ya mashine ya Sh2m itakayo tumika kupima ugonjwa wa kifua kikuu kuezekwa kwenye hospitali ya Manga kwa ufadhili wa Wizara ya Afya nchini.
Akihutubia wanahabari hospitalini Manga, mshirikishi wa huduma za ugonjwa wa kifua kikuu nchini, Bw Jeremiah Okari alisema kwamba mashine hiyo itasaidia kufanya vipimo vya ugonjwa huo kwa muda mfupi ili kuwawezesha madaktari kuwapa dawa watakao patikana wameathirika.
"Mashine ambayo tumeiezeka kwenye hospitali ya Manga hii leo itawawezesha wananchi kufanyiwa vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu na kupokea majibu kwa haraka ili madaktari waweze kuwapa dawa wale watakao patikana kuathiriwa," alisema Okari.
Okari alisema kuwa kaunti ndogo ya Manga ni miongoni mwa sehemu zinazosajili viwango vya juu vya ugonjwa wa kifua kikuu na kuwaomba wakazi kujitokeza ili kupimwa ugonjwa huo.
"Sehemu hii ya Manga ni moja wapo ya sehemu zinazo rekodi viwango vya hali ya juu kwa watu walio athirika na ugonjwa wa kifua kikuu na ndio maana nawaomba wakazi kujitokeza kupimwa ili kujua hali zao," alisema Okari.
Afisa mshirikishi wa maradhi ya kifua kikuu kwenye Kaunti ya Nyamira alisema kuwa mashine hiyo ni ya tatu sasa kuezekwa kwenye kaunti ya Nyamira kwa kuwa mashine kama hizo mbili tayari zimeezekwa kwenye hospitali ndogo ya Nyansiongo na hospitali kuu ya Nyamira.
Muma aliwarai wakazi kuwa kwenye mstari wa mbele kuhakikisha kuwa visa vya ugonjwa huo vimepungua kwa kuwahimiza walio na kikohizi kilicho dumu zaidi ya wiki moja kutembelea vituo vya afya kupimwa na kujua hali zao.
"Nawasihi wakazi wa eneo hili kuwahimiza wale ambao wamekuwa na kikohozi kinacho zidi wiki moja kutembelea vituo vya afya ili kupimwa na kujua hali zao,” alisema Muma.
Aliongezea: "Kaunti ya Nyamira ina idadi ya wananchi wapatao elfu 6078, 587 lakini kati ya idadi hii yote, ni asilimia kumi tu kati yao wanao jua hali zao jambo ambalo ni la kishangaza sana.