Naibu Gavana wa kaunti ya Kisii Joash Maangi amewaomba viongonzi wote kushirikiana ili kuinua viwango vya maendeleo katika kaunti ya Kisii.
Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi yake siku ya Jumatatu, Naibu Gavana wa Kaunti ya Kisii Joash Maangi aliwaomba viongozi wote wa kaunti ya Kisii kushirikiana ili kuinua uchumi wa kaunti hiyo.
Maangi alisema kuwa ushirikiano ni njia mojawapo ya kuinua uchumi wa Kaunti yua Kisii ili kaunti hiyo iweze kujiendeleza kimaendeleo kwa kuwa kuna ushidani mkubwa kati ya kaunti zote 47.
Kwa sasa amewaomba viongozi waliomamlakani kushirikiana haswa katika miradi mbalimbali kama masomo na miradi ya kuendeleza maendeleo katika kaunti hiyo.
Maangi alisema yeye kama naibu gavana atashirikiana na Gavana wake James Ongwae ili kuhakikisha kuwa serikali ya kaunti ya Kisii imeendelea kusonga mbele kwa kuchukua hatua ya kimaendeleo ili wakazi waweze kufaidika.
Aidha, aliwaomba viongioni wote kuungana na kufanya kazi pamoja ili mwananchi wa kawaida aweze kusaidika.
“Naomba viongozi wote waje pamoja ili tushirikiane kwa kuendeleza kaunti yetu kwa kuwa sisi kama viongozi tuna wajibu wa kufanya kazi kwa wananchi," alisema Maangi.
Alisema kuwa wao kama viongozi ndio wanastahili kuwa na mwongonzo kwa wananchi haswa katika miradi ya maendelea ya kuwasaidia watu hao.
Maangi ambaye ni mwenyekiti wa manaibu magavana nchini alisema kuwa atahakikisha kuwa serikali za kaunti zinalindwa na kujiendeleza kimaendeleo.