Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini, Kaunti ya Kisii wamempongeza mbunge wa eneo bunge hilo Jimmy Angwenyi kwa kulikarabati barabara ya kilomita 54.

Hii ni baada ya barabara hii kutatiza shughuli za uchukuzi kwa muda mrefu haswa kunaponyesha, lakini kwa sasa wakazi wa eneo hilo wana kila sababu ya kufurahia baada ya kilio chao kusikizwa na mbunge wa eneo hilo.

Wakizungumza na Waandishi wa habari siku ya Jumanne katika eneo la Marani, wakazi hao wakiongozwa na Ezekiel Nyagaka walimpongeza Mbunge Angwenyi kwa kulikarabati barabara hilo la kutoka eneo la Kegogi-Ngongoro-Sombogo-Marani.

“Tunamshukuru mbunge kwa yale yote ameyatekeleza maanake hayo ndio maendeleo tunayohitaji,” alidokeza Julius Moreka, mkazi.

Wakati uo huo, wakazi hao walimuomba mbunge huyo kujaribu kila awezalo kabla ya awamu yake mamlakani kuisha kuhakikisha barabara hilo limewekwa lami kwani ni mojawapo ya barabara ambazo naibu Rais William Ruto alisema ziwekwe lami wakati alipozuru eneo hilo la Marani kwa takribani mienzi mitatu ziliyopita.