Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa eneo bunge la Mugirango Kusini Kaunti ya Kisii Manson Oyongo Nyamweya ameombwa kuwajibika katika kazi yake viilivyo na kuwaletea wakaazi wa eneo hilo maendeleo.

Akizungumza siku ya Jumanne katika uwanja wa shule ya msingi ya Tabaka ilioko eneo bunge hilo la Mugirango Kusini, mwenyekiti wa bodi ya kuwaajiri wafanyikazi katika kaunti ya Kisii David Kombo alidai kuwa mbunge huyo hajawajibika katika kazi yake huku akimkosoa kwa kutopeleka huduma ya vijana ya (NYS) katika eneo bunge hilo ili wapate kazi kama maeneo bunge mengine.

“Namwomba mbunge wa eneo hili Manson Oyongo kuleta maendeleo katika eneo hili. Mambo ya kutangaza kuwania kiti cha ugavana aweke kando afanye maendeleo kwanza,” alisema Kombo.

Aliongezea: “Maeneo bunge yote yanafanya shughuli ya kuwaajiri vijana katika huduma ya NYS lakini hapa kwetu hakuna shuguli kama hizo. Wacha tuweke siasa kando tufanye maendeleo maana wananchi wa eneo bunge hili wanahitaji maeneleo."

Wakaazi wa eneo hilo waliuunga mkono mwenyekiti huyo huku wakisema wanahitaji barabara zote za eneo hilo ziwekwe lami kupitia hazina ya ustawi ya maeneo bunge kabla ya kuwania kiti cha ugavana katika kaunti ya Kisii.

“Tunaomba mbunge Nyamweya afanye maendeleo haswa kwa kutengeneza barabara kwa kuziweka lami kisha akifanya hivyo atangaze anachohitaji lakini kwa sasa asubiri tupate maendeleo kwanza,” alisema Peterson Siro, mkaazi.