Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mpango wa kuwachanja mifugo ili kuzuia magonjwa mbalimballi ya mifugo umeanzishwa wilayani Borabu kaunti ya Nyamira.

Akizungumza siku ya Jumatatu, afisa anayesimamia kutibiwa kwa mifugo wilayani Borabu Dkt Isaiah Chacha, alisema mpango huo unanuia kufikia mifugo kama ng’ombe, kondoo, mbuzi, mbwa na hata paka.

"Mifugo kuanzia ng'ombe, mbuzi, kondoo, punda, mbwa na paka miongoni mwa wengine watapokea dawa na hiyo itakuwa njia ya kudhibiti magonjwa kama ya midomo, miguu na mengineyo ambayo hukumba mifugo,” alisema Dkt Chacha.

Aidha, daktari huyo amewahimiza wakazi wilayani Borabu kuhakikisha kuwa mifugo wao wamepata chanjo hiyo ili kuzuia vifo vya mifugo.

Mpango huo utaendeshwa kwa kipindi cha wiki moja.

"Nawaomba wakazi kuhakikisha kuwa mifugo wao wamepokea chanjo hiyo ili kuzuia vifo ambavyo husababishwa na magonjwa hayo," aliongezea Dkt Chacha.