Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwanamume anayekabiliwa na mashtaka ya kulawiti mtoto wa miaka 14 ametozwa dhamana ya shilingi 300,000 katika mahakama ya Mombasa.

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatano, hakimu wa mahakama ya Mombasa Susan Shitub alisema kuwa ni haki kwa kila mshukiwa kupewa dhamana kwa mujibu wa katiba.

Mshukiwa huyo, Bonifance Mbuki, alikanusha madai hayo na kusisitiza kuwa hakuhusika kamwe.

Mbuki alisalia korokoroni kwa siku sita tangu kutiwa mbaroni, baada ya afisa wa upelelezi Martin Ojwang kuiomba mahamaka siku ya Alhamisi kumpa mda zaidi wa kukamilisha uchunguzi wake, kabla ya kumfungulia mashtaka mshukiwa huyo.

Ojwang alielezea mahakama kuwa mshukiwa anadaiwa kumlawiti kijana huyo tarehe 16 Oktoba katika eneo la Mtongwe huko Likoni na kisha kutoroka.

Mahakama ilielezewa kuwa maafisa wa polisi kwa ushirikiano na wananchi walifanikiwa kumtia mbaroni mshukiwa huyo tarehe 21 Oktoba katika eneo hilo la Mtongwe.

Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 24, 2015.