Mwanamume mmoja wa umri wa miaka 40 kwa jina Peter Manyasi kutoka kijiji cha Kiombati, wilayani Manga alijitia kitanzi usiku wa kuamkia siku ya Jumatano.
Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, mwanamume huyo amekuwa akiishi kwa kero na changamoto chungu nzima baada ya mke wake kuhama na kwenda kwao na kumwacha peke yake, jambo ambalo linasemekana kumtia hofu na kumchukulia kujitoa uhai wake.
Dancan Bosire, mwanakijiji, alisema mwanamume huyo hakuwa anaonyesha dalili ya kujitoa uhai ila alikuwa na usumbufu wa fikira za mkewe kwa kuhama na watoto wake wawili.
Visa vya kujitoa uhahi katika kaunti ya Nyamira vimekuwa vikiongezeka kila kuchao, huku wengine wakiendelea kuuliwa.
Wanakijiji hao waliskitishwa ni kitend hicho na kukilahani pakubwa, huku wengine wakisema ikiwa mtu ana shida, anastahili kuzungumza na watu na kuomba usaidizi.
“Tunaomba yeyoyote mweye shida kabla ya kufikiria kujiua anastahili kulileta lile jambo ambalo linamsumbua kwa wazee ili kulizungumzia,” alisema Gladys Chae, mwanakijiji.
“Hatujui ni nini kimekuwa kwa watu ambao wanaona kujiua huenda kukawa ni suluhu kwa maisha yao, tunaomba hiyo tabia ikome maana ni laaana hata kwa wale wanabaki ambao ni wa ukoo mmoja,” aliongezea Chae.
Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Nyamira walisafirisha mwili wa marehemnu hadi chumba cha kuhifadhi maiti cha Nyamira, huku uchunguzi ukiendelea kufanywa kuhusiana na kisa hicho