Mwanamume wa umri wa makamo siku ya Alhamisi alishtakiwa kwa kosa la kumchomea mamake nyumba baada naya kuzozana na ndugu zake.
Mwanamume huyo aliyetambulika kama Dourghat Imbisi alikana mashtaka mbele ya hakimu mkuu, Irene Wema huku akiielezea mahakama kuwa alijawa na ghadhabu pale baadhi ya jamaa zake walimtaka ahame katika boma hilo ilhali hakuwa na mahali pa kwenda.
Imbisi amedaiwa kutenda kosa hilo siku ya Jumapili mwezi wa Agosti 23, katika shamba la mamake, Celestine Imbisi, Wilayani Kisii.
Mahakama ilimwachilia Imbisi kwa dhamana ya shilingi 100,000 au pesa taslimu 50,000 huku kesi ikiahirishwa hadi tarehe 5 mwezi wa Oktoba.
Hata hivyo, rabsha ilizuka nje ya mahakama pale ndugu zake mshukiwa huyo walitaka kumpa adhabu kwa kumpiga lakini askari waliokua wakishika doria nje ya mahakama waliwazuia na kuwafukuza.