Mwanamke mmoja wa umri wa makamo amefikishwa katika mahakama moja mjini Nakuru leo Alhamisi kwa tuhuma za kumuibia mama yake gunia mbili za mahindi na kisha kumuunguza kwa chai.
Korti ilielezwa kuwa mnamo mwezi Mei tarehe 21 mwaka huu, Paul Kamau alimuunguza mamake kimaksudi akitumia chai ya moto katika kijiji cha Likia, Wilayani Njoro katika Kaunti ya Nakuru.
Mshukiwa huyo hata hivyo aliyakana madai hayo mbele ya mahakama hiyo. Mamake Esther Kamau alinusurika kupitia kwa mwanawe wa kike na kupelekwa katika hospitali ya Njoro alikouguza majeraha aliyoyapata kufuatia kitendo hicho cha kinyama.
Mshtakiwa aliomba mahakama iweze kumuachilia huru kwani alikuwa ndiye kitega uchumi cha jamii yake na zaidi ya hayo mke wake alikuwa mjamzito huku watoto wakihitaji karo.
"Nina watoto watatu wanaonitegemea na ninaomba mahakama inionee huruma kwa kuniachilia huru kwani hata mke wangu ni mjamzito," alisema Kamau.
Hata hivyo, kilio chake kiliambulia patupu kwani Hakimu Mkuu Doreen Mulekyo alikidunisha na kusema kuwa mtuhumiwa ana kesi ya kujibu na ni sharti awajibikie makosa aliyoyafanya.
Paul ataendelea kusalia korokoroni hadi pale kesi yake itatajwa tena.