Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanasiasa aliyewania kiti cha ubunge katika eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini kaunti ya kisii, James Atandi amemtaka mbunge aliye mamlakani katika eneo bunge hilo Jimmy Nuru Angwenyi kuheshimu wanasiasa wengine walio katika mamlaka na wale wasio mamlakani.

Akizungumza siku ya Alhamisi katika hafla ya mazishi ya ajuza Jeruza Orure yalioyofanyika katika kijiji cha Kemanko, Atandi alimtaka mbunge wa eneo hilo kutoharibia majina wanasiasa wengine na kufanya kazi aliyochaguliwa kufanya.

"Sisi wanasiasa ni maadui kwa wanasiasa wengine. Ni jukumu la kila mwanasiasa kuheshimu mwanasiasa mwingine. Naomba mbunge wa eneo hili kuniheshimu ingawa zikuchaguliwa. Wakati wangu utafika na mwaka 2017 nitasimama tena. Angwenyi asije akaniharibia jina kwa mikutano mingine,”alisema Atandi. 

Aidha, mwanasiasa huyo aliomba mbunge wa eneo hilo jimmy Angweny kuonyesha uwazi wakati pesa za msaada wa karo kutoka hazina ya CDF zinapopokezwa kwa wanafunzi wa eneo bunge hilo.

“Kila mwanafunzi anastahili kupokezwa pesa za msaada wa karo lakini kuna maneno ambayo hufanyiwa mvunguni. Wale waliojulikana wakati wa kampeini watoto wao ndio hufaidika na hupokezwa pesa hizo. Niko na fomu nyingi ambazo zinaonesha mambo hayo na zinafichua ukweli wa pesa hizo. Nitayafichua mambo hayo hivi karibuni ili yajulikane,” aliongeza Atandi.

Kwa upande mwingine watu waliokuwa katika mazishi hayo walimshangilia mwanasiasa huyo huku wakisema ni ukweli yale aliyokuwa akisema haswa kuhusu ugawaji wa pesa za msaada wa karo katika eneo bunge hilo.