Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanasiasa Victor Swanya kutoka eneo bunge la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira ameomba serikali kuhakikishia wananchi wa eneo bunge hilo usalama wa kutosha.

Hii ni baada ya mfanyibiashara mmoja kutoka wadi ya Mochenwa kushambuliwa siku ya Jumatatu usiku alipokuwa anaelekea nyumbani kwake kutoka mahala anapofanyia biashara yake na kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana.

Jambo hilo lilimpelekea mwanasiasa huyo kuingilia kati na kuomba serikali kuimarisha usalama wa kutosha katika eneo hilo ili watu wengi wasiendelee kujeruhiwa na majambazi.

Kisa kama hicho si cha kwanza kushuhudiwa katika eneo hilo, kwani visa vitano sasa vimeripotiwa, huku usaidizi ukiombwa kutoka kwa serikali kwani watu wengi wamehofya usalama wao.

Akizunguma siku ya Jumanne katika wadi ya Mochenwa mwanasiaa, Swanya alishangazwa kwa nini serikali haitaki kuimarisha usalama katika eneo hilo, huku watu wengi wakiendelea kusumbuliwa kila kuchao.

“Ninaomba serikali kuimarisha usalama katika eneo bunge hili la Kitutu Masaba kwani visa hivi vimekuwa vingi na serikali iko ambayo inastahili kuimarisha usalama kwa wananchi,” alisema Ogeto.

Matamshi yake yaliungwa mkono na idadi nyingi ya wananchi wa wadi ya hiyo na walipendekeza idadi ya maafisa wa polisi kuongezwa ili kuimarisha usalama.