Wakazi jijini Mombasa wamelitaka Shirika la kudhibiti mazingira Nema, kuingilia kati na kuonya baadhi ya wakazi dhidi ya kucheza muziki wa sauti ya juu katika majumba na magari yao.
Wakizungumza Siku ya Alhamisi, wakazi hao walisema wanasumbuliwa na muziki huo hasa nyakati za usiku ikizingatiwa huo huwa wakati wao wa kupumzika baada ya shughuli za kutafuta riziki.
Mmoja wa wakazi hao Athuman Salim kutoka mtaa wa Kongowea, alisema kuwa anasikitishwa na kukerwa na baadhi ya majirani wake wanao cheza muziki kwa sauti ya juu nyakati za usiku bila kujali masilahii ya wengine.
Aidha, aliongeza kuwa ngoma za matanga zifutiliwe mbali hasa nyakati wa usiku kwani zimezidi hasa katika sehemu mbali mbali za eneo hilo.
“Wanaocheza muziki kwa sauti ya juu wanafaa kutiwa mbaroni kwani wanatusumbua,” alisema Salim.