Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakazi wa Nyamira wamempongeza seneta wa kaunti hiyo Kennedy Okong’o kwa kumlipia mmoja gharama ya hospitali.

Aliyelipiwa gharama ya hospitali katika hospitali ya Nyamira Level Five Alice Nyaboke alikuwa amemaliza muda wa miaka mitatu kwa sababu ya kushindwa kulipa gharama za matibabu.

Hii ni babada ya Nyaboke kutoka eneo la Nyabite ambaye pia ni mlemavu alienda kujifungua mtoto mwaka wa 2013 na kwa bahati mbaya hakuwa na pesa za kulipa katika hospitali na kumlazimu kuweka makao katika hospitali, jambo ambalo limefika mwisho baada ya Seneta Okong'o kumlipia gharama zote kufikia siku ya Jumanne.

Wakizungumza na Waandishi wa habari siku ya Jumanne katika mji wa Nyamira, wakazi hao wakiongozwa na Linet Omanwa walimpongeza Seneta Okong’o kwa kulipa pesa zote katika hospitali hiyo na kusema wanahitaji viongonzi wa aina hiyo ambao husaidia wananchi.

“Huyu mama amekuwa akikita kambi katika hospitali hii kwa miaka mitatu baada ya kushindwa kulipa gharama ya matibabu. Namshukuru Seneta wetu Okong’o kwa moyo wake mkunjufu wa kusaidia na tunamwomba aendelee na usaidizi wa aina hiyo.

Wakati uo huo, Seneta Okong’o alisema alimjengea nyumba ambayo hakuwa nayo kwani mume wa mwanamke huyo alimfukuza, hali ambayo ilimuacha bila mahala pa kuweka makao tena.

“Seneta wetu amefanya kazi nzuri sana ya kulipia mama huyo gharama ya hospitali na kumjengea nyumba. Mungu ambariki sana na amzidishie maisha,” alisema David Moku,a mkazi