Wanabiashara katika soko la Daraja Mbili mjini Kisii wameiomba serikali ya kaunti ya Kisii kutimiza ahadi yake ya kuwajengea vibanda katika soko hilo.
Wakiongea hii leo Jumatatu katika soko hilo, wanabiashara hao walisema wanasubiri kujengewa vibanda hivyo kutokana na ahadi ya serikali ya kaunti ili waweze kusaidika haswa wakati wa jua kali au at mvua.
Wanabiashara hao walisema kuwa wanavumilia jua kali na mvua katika soko hilo, jambo ambalo husababisha hasara kubwa kwa biadhaa zao kuharibika.
Aidha walisema kuwa vibanda hivyo vitawasaidi kila mtu kujua mahali pa kuuzia, kwani kwa sasa kila mtu huweka bidhaa zake mahali anataka.
Vellah Nyaboke ni mmoja wa wanabiashara hao ambaye alisema kuwa vibanda katika soko hilo vinahitajika kwani tangu soko hilo lianzishwe hawana mahali pa kuweka bidhaa zao .
“Naomba serikali ya kaunti yetu ya Kisii kutimiza hadi zake na kutujengea vibanda hivyo ili nasi tuweze kunufaika bila kupata hasara,” alihoji Mama Nyaboke, mwanabiashara wa Nyanya.
Kwa upande wa usafi, wafanyabiashara hao walisema kuwa serikali ya kaunti Imewasidia pakumwa kuwa uwepo wa vijana wanaofagia soko hilo na kuhakikisha kuwa kila kuchaoao soko hilo ni safi.