Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Shughuli katika kiwanda cha kutengeneza vileo cha Keroche zilitatizwa Jumatano baada ya kundi la vijana kujaribu kuharibu bidhaa zao.

Fujo ilizuka vijana hao walipokabiliwa na askari wakupambana na ghasia kwenye lango kuu la kampuni hiyo. Vijana hao  walitaka kuingia ndani wakisema vileo vinavyotengenezwa na kampuni hiyo havijafikia kiwango kinachokubalika.

Kamishna waeneo la bonde la ufa Osman Warfa na mbunge wa Naivasha John Kihagi ndio walioruhusiwa kuingia kwenye kampuni hiyo. 

Maafisa wa halmashauri ya ubora wa bidhaa nchini (KEBS) walifunga shughuli za kampuni hiyo kufuatia hasira ya wasimamizi waliowashutumu kuongoza operesheni hiyo.

Baada ya muda ilimbidi mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Tabitha Karanja kuamuru wafanyikazi, maafisa na mbunge Kihagi kuondoka. Karanja alimlaumu mbunge wa eneo hilo kwa kuingiza siasa kwa shughuli za kampuni hiyo.

Aliongeza kuwa aina ya pombe waliokuwa wakitengeneza kamwe haikuwa imeorodheshwa kama pombe haramu na kusema kuwa wanaendeleza shughuli za utengenezaji vileo kwa mujibu wa sheria. 

"Biashara yetu ni halali, hatutawaruhusu wahuni kuharibu mali yetu kwa madai yasiyodhibitishwa," alisema.

Kihagi alisema hana nia yoyote mbaya dhidi ya kiwanda hicho.