Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Vijana 30 kutoka kaunti ya kisii wametunukiwa taji ya kuhitimu kwa kupokea mafunzo ya teknologia ya kisasa ambayo ni ya kidigitali ili kuwawezesha vijana hao kuwafundisha vijana wengine masuala ya mawasiliano ya teknologia katika kaunti hiyo.

Hii ni baada ya mafunzo hayo kuandaliwa na Elizabeth Ongwae ambaye ni mkewe Gavana wa kaunti ya kisii James ongwae akishirikiana na shirika moja lisilo la serikali 'Digital opportunity Kenya'.

Vijana hao walihitimu siku ya Jumatatu katika uga wa gusii huku Elizabeth Ongwae akiwavisha vijana hao wote taji hizo ili wajiendeleze kimaisha kwa masuala ya kidigitali.

Vijana hao waliopokea mafunzo hayo ya teknologia walikua wa miaka kati ya 18 hadi 30 ambao hawakupata fursa ya kujiunga na vyuo baada ya kumaliza kidato cha nne na kukaa nyumbani bila kufanya chochote.

“Hii ni njia mojawapo ya kuwapa fursa vijana wetu kujua mambo ya teknologia ya kisasa katika kaunti yetu. Leo tunawakabidhi vijana hawa vyeti vyao na baada ya hapa tutawatafutia njia ya kuwapa pesa ili waanzie kufanya biashara ili tupungunze umaskini,” alisema Elizabeth Ongwae.

Aidha, mkewe ongwae alisema mradi huo wa kuwapa vijana mafunzo ya teknologia utaendelea kufanyika katika kaunti ya kisii ili vijana wasije wakajiunge na mambo ya kubugia pombe baada ya kukosa cha kufanya.

“Hawa vijana tutawatafutia kazi ya kufanya na kutoka hapo tutawapa pesa wafanyie biashara haswa biashara ya masuala haya ya teknologia ili wajiendeleze kimaisha,” aliongeza Elizabeth Ongwae.