Kutokana na kushuhudiwa idadi kubwa ya makahaba nyakati za usiku jijini Mombasa, vijana wa Kiislamu wamehimizwa kuoa mapema ili kujiepusha na maovu hayo.
Akizungumza kwenye maombi katika Msikiti wa Konzi siku ya Ijumaa, ustadhi Mohammed Lali alisema kuwa ili kupunguza idadi ya makahaba na ugonjwa la ukimwi jijini Mombasa, basi ni wajibu kwa wazazi kuwaoza watoto wao pindi tu wanapotimiza umri wa kuolewa.
Aidha, aliwasihi wazazi kupunguza kiwango cha mahari ambayo huwa changamato kubwa inayo wafanya vijana kukosa kuoa hivyo basi kuwafanya kushiriki ngono ovyoovyo.
“Waozeni watoto wenu pindi wanapotimiza umri wa kuolewa na kuoa ili kupunguza maovu ya ngono za mapema zinazo shuhuidiwa jijini,” alisema Lali.
Vile vile Lali aliwataka wazazi kuwajibika katika malezi bora ya watoto wao kama njia moja wapo ya kuepuka biashara hiyo ya ngono.
Makahaba wengi hasa wa umri mdogo huonekana katika maeneo ya Sabasaba, Kongowea na kwengineko wakishiriki katika biashara hiyo wakati wa usiku.