Share news tips with us here at Hivisasa

Shughuli ya huduma ya kitaita ya vijana al maarufu NYS kuimarisha na kubadilisha maisha ya wakenya wanaoishi maisha duni imeanza hii leo (Alhamisi) katika eneo Bunge la Kitutu Chache Kusini.

Akizindua mikakati hiyo hii leo katia eneo la Mosocho, Mbunge wa Kitutu Chache Kusini Richard Momoima Onyonka ameapa kuwapa vijana hao lolote watakalohitaji ili kufanikisha shughuli hiyo.

"Nina furaha sana kwa kuona vijana wamejitokeza kwa wingi na nina imani kuwa vijana wa eneo hili letu wanatamani sana kuishi maisha ya kupendeza na kubadilisha sura ya Kitutu Chache Kusini," alisema Mbunge Onyonka akiongezea kuwa atakua nao hadi watakaotamatisha shughuli hiyo kikamilifu ili maeneo mangine yaige kama mfano mwema.

Aidha, Onyonka ameipongeza Serikali Kuu kwa miradi hiyo ya aina ya kipee kama huo wa kuhakikisha wananchi wana makaazi ya kufana na yaliyo na mazingira masafi kote nchini.

Amewarai vijana kuwa katika mstari wa mbele kimaendeleo na kuepuka na siasa duni akisema wakati wa siasa ungali bado haujafika kwa sasa.

Amewataka vijana hao kujiunga na kuunda makundi ya kijamii na kuyasajili ili wanufaike kutokana na mipango ya Serikali ya Kaunti ya Kisii na ile ya taifa.

Mamia ya vijana walijitokeza kushiriki katika mradi huo wa kuimarisha maisha ya wakaazi wa eneo bunge hilo likiwa miongoni mwa mengine ya kwanza kutekelezwa katika maeneo ya Magharibi mwa Kenya.