Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Viongonzi wa Kaunti ya Kisii wanatarajiwa kukutana kujadili jinsi ya kuongoza na kuinua viwango vya maendeleo katika kaunti hiyo.

Akiongea siku ya Jumapili katika hafla ya mchango wa kusaidia Shule ya Wavulana ya Nyamache katika shule hiyo ilioko eneo bunge la Bobasi katika Kaunti ya Kisii, Seneta wa Kaunti ya Kisii Chris Obure alisema kuna umuhimu wa viongozi kutoka eneo la Kisii kukutana ili kuweka mikakati ya kuendeleza kaunti hiyo kimaendeleo.

“Kaunti yetu haitasonga mbele kimaendeleo ikiwa sisi kama viongonzi wa hapa hatutakuja pamoja na kuweka mikakati ya kuiendeleza haswa kimaendeleo,” alihoji Seneta Obure.

Aidha, alisema atahakikisha kuwa wabunge na viongozi wengine watafika kwenye mkutano huo ambao alisema unatarajiwa hivi karibuni kujadilia masuala muhimu ya kuinua kaunti huku akimuomba Gavana James Ongwae pia kuwaweka viongonzi wa kaunti ya Kisii pamoja ili waweze kukutana pamoja.

Seneta Obure alisema kaunti hiyo haiwezi kusonga mbele kimaendeleo ikiwa viongozi hawatakuja pamoja na kuweka mikakati ya kuiendeleza kimaendeleo.

Kwa upande wake, Gavana Ongwae aliyekuwa kwenye hafla hiyo alipongeza hatua hiyo na kusema yupo tayari kukutana akiongeza kuwa atahakikisha Wawakilishi katika bunge la kaunti hiyo watakutana na Wabunge ili kujadiliana na kuweka mikakati kapambe ya kuinua Kaunti ya Kisii kimaendeleo.