Waendeshaji bodaboda wa eneo la Gichauri katika Bunge la Borabu, Kaunti ya Nyamira wamepokezwa cheti chao (Borabu Bodaboboda Sacco Certificate) ambacho kitawasaidia kupokezwa mikopo kutoka hazina mbalimbali.
Akiongea siku ya Jumapili katika eneo la Gichauri alipowapokeza waendeshaji bodaboda hao cheti hicho, wakili Alfaxard Osoro aliwaomba kutotegemea kazi za kuajiriwa na kutafuta mbinu ya kujisaidia kwa kutafuta pesa wao wenyewe ili kujiimarisha kimaisha.
Wakati uo huo, wakili Osoro alisema cheti hicho kitawasaidia kupata mikopo na kuwanunulia wale hawana pikipiki zao wazitumike kufanya biashara na kurudisha pesa za mikopo na kubaki na pikipiki zikiwa zao.
Wakili huyo alifurahishwa na waendeshaji bodaboda wa Gichauri kwa motisha waliyo nayo kwa kutia bidii kutafuta pesa kupitia uchukuzi wao na kutafuta pesa ambazo zitawasaidia nyakati zijazo.
Pia wakili Osoro aliwanunulia waendeshaji bodaboda hao tarakilishi na ‘printer’ ambayo itakaa katika ofisi ya waendeshaji bodaboda hao.
Waendeshaji bodaboda hao walimpongeza wakili Osoro kwa usaidizi aliutoa kwao na kuahidi watajaribu wawezalo kujiendeleza kimaisha kwa kujitafutia pesa na kujisaidia kama njia moja ya kujiendeleza kimaisha.
“Ni ahsante tunasema kwa yale wakili Osoro ametupa maana amaetusaidia sana na tumetoka mbali kupitia yeye na sisi tutajaribu kujiendleza,” alisema Victor Omwoyo, mwendeshaji bodaboda.