Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Waendeshaji bodaboda katika eneo la Ogembo, eneo bunge la Bobasi ambao waliandamana siku ya Jumatatu wakilalamikia uongozi mbaya wa Gavana wa Kaunti hiyo James Ongwae.

Waendeshaji bodaboda hao walidai kuwa Gavana Ongwae hafanyi kazi sawia na sehemu zingine zilizoko katika kaunti hiyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu walipokuwa wakiandamana katika eneo hilo la Ogembo, waendeshaji bodaboda hao wakiongonzwa na Peter Osiemo walidai kuwa Gavana Ongwae hajawajibika kikamilifu kwa kufanya maendeleo katika kaunti nzima ya Kisii.

Haya yanajiri baada ya ajali kutendeka katika eneo hilo la Ogembo na kugharimu maisha ya watu wanne kwa ukosefu wa kituo cha magari ambacho magari yatakuwa yakipangia abiria.

Wakati huo huo, chama cha eneo bunge la Bomachoge kwa jina ‘consultative Forum’ ambacho huwaleta pamoja wafanyikazi wote wa kaunti ya Kisii na wale wa serikali ya kitaifa wakiongonzwa na mwenyekiti wao John Oyaro walijitokeza na kulaani maandamano hayo.

Aidha John Oyaro alidai kuwa  Naibu gavana wa kaunti ya Kisii Joash Maangi ndiye alipanga maandamano hayo jambo ambalo alisema liliwakera sana na kusema uchungunzi unapaswa kufanywa na hatua ya haraka ichukuliwe dhidi yake.

“Tunajua kuwa ni naibu gavana aliyepanga maneno haya ya maandamano. Sisi tunasema alifanya vibaya sana na tunampenda gavana wetu James Ongwae,” Oyaro.