Share news tips with us here at Hivisasa

Wafugaji wa ng’ombe za maziwa kutoka kijiji cha Kiamitengi, wadi ya Gesima wameiomba serikali ya kaunti ya Nyamira kuwatafutia soko la maziwa.

Wakiongea siku ya Jumatano katika eneo la Bokione wakati walikutana na kikundi kimoja ambacho kinataka kuazisha kununua maziwa katika eneo hilo, wakaazi hao waliiomba serikali ya kaunti ya Nyamira kuwatafutia soko ili kujiendeleza na ufugaji wa Ng’ombe.

Aidha, walisema wanapata hasara kubwa maana hakuna soko la maana la kuuza maziwa, na lile liko linanunua kwa kiwango cha chini au wanakosa kununua kabisa.

Wakulima hao walisema kulikuwa na kampuni moja ambayo ilikuwa ikiwasaidia kununua maziwa hayo siku za nyuma, lakini tangu ifungwe wakulima hao wamekuwa wakiangaika na maziwa yao bila kuwa na mahali pa kuuza .

“Mimi huwa nakamua ng’ombe wangu watatu lita 12 kila siku na sina soko la kuuza maziwa hayo, naomba serikali yetu ya Nyamira kututafutia soko ili nasi tuweze kujiendeleza na ufugaji na kupata faida kutoka kwa ng’ombe hao,” alihoji Mokeira Edina, mkulima.

Kwingineko, wameomba serikali hiyo kutimiza ahadi iliyotoa ya kutoa ng’ombe za maziwa kwa kila wadi kama njia moja ya kuendeleza ufugaji.

“Naomba serikali ya kaunti kutimiza ahadi iliyotoa ya kutoa ng’ombe za maziwa kwa Kila wadi,” alihoji Kalvin Basweti.