Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wafanyikazi wa kubebe mizigo kwa kutumia mkokoteni  katika Kaunti ya Kisii wamewaomba wahudumu wa magari kuwaheshimu ili nao waweze kujiendeleza kimaisha na biashara zao kwani nao wanatafuta riziki.

Wakiongea siku ya Ijumaa na Mwaandishi  huyu katika mtaa wa Mwembe, Wadi ya Kisii ya kati katika Kaunti ya Kisii, baadhi ya wahudumu hao wamewalaumu baadhi ya wahudumu wa magari haswa madereva na kuwaomba kuwaheshimu na kuheshimu wakiwa barabarani ili wapate mapato yao ya kila siku.

Kwa mujibu wa wahudumu hao wa mkokoteni, baadhi ya madereva huwaona kuwa wao si watu wakati wapo kwenye barabara wakisafirisha mizigo ya wateja wao.

“Nikiwa barabarani na gari linatoka nyuma huwa ninapigigwa honi kila mara kiashirio kuwa nitoke ili gari hilo liweze kupita na huwa nashangazwa sana kwani sisi si haki kutumia barabara kama wenzetu," alihoji Fred Mochache, mhudumu wa mkokoteni mjini Kisii.

Kwa sasa wahudumu hao wa mkokoteni  wamewaomba wenzao wa sekta ya matatu kujua kuwa nao wanafanya kazi  kama wengine  na wanatafuta sabuni ya kila siku na kuongeza kuwa lazima kazi ya kila mtu iheshimiwe kwani kazi ni kazi.

“Kila mtu katika dunia hii anatafuta kwa hivyo ni vyema wenzetu kujua kuwa hata sisi tunatafuta sabuni kama wao tu na sisi sote tupo chini ya sekta ya uchukuzi," alihoji Daniel Basweti, muhudumu mwingine wa mkokoteni mjini humo.