Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakaazi wa wadi ya Birongo na wadi ya Keumbu wameombwa wawe wanalipia gharama ya maji kila mwezi kama njia moja ya kujiepusha na madeni na kampuni ya maji.

Haya yanajiri baada ya serikali ya kaunti ya Kisii kupitia uongozi wa Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae,  kuahidi kulipa deni la shillingi million tano ya maji ambayo ilipelekea maji hayo kukatwa na kampuni inayosimamia maji hayo na kuwaacha wananchi wakihangaika bila maji kwa muda mrefu. 

Serikali ya Kaunti ya Kisii imeamua kuwasaidia kulipa deni hilo ili wakazi hao waweze kujiendeleza haswa katika sekta ya kilimo ambayo inahitaji maji.

Wakiongea siku ya Jumanne katika wadi ya Birongo, wakaazi wa maeneo hayo walisema kuwa wamekuwa wakiteseka kwa ukosefiu wa maji kwa muda mrefu tangu kukatwa kwa maji hayo ambayo walikuwa wanategemea. Waliipongeza serikali ya kaunti kwa kuwasaidia kulipa deni hilo ili waweze kunufaika na maji. 

Aidha, baadhi ya wakaazi waliwaomba wenzao kuwajibika kuwa wakati wamewekewa maji lazima wawee wanalipia maji hayo kama njia moja ya kujiepusha na deni.

“Naomba wenzagu kuwa tutakapounganishiwa maji haya, nasi iwe wajibu wetu kulipia kila mwezi kwani maji haya hutusaidia pakumbwa na ninaipongeza serikali ya kaunti ya Kisii kwa kutukumbuka,” alisema Zachariah Onyoni, mkaazi.