Mkuu wa Tarafa ya Gesima Vincent Koech amewaomba wakaazi wa eneo hilo kushirikiana na utawala wa tarafa hiyo ili kumaliza ukosefu wa salama katika eneo hilo.
Akiongea na wakaazi wa Tarafa ya Gesima, eneo Bunge la Kitutu Masaba,Kaunti ya Nyamira katika hafla ya baraza iliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Nyabiosi siku ya Jumatano, Koech aliwaomba wakazi wote kushirikiana na Machifu na Naibu wao ili kuinua viwango vya usalama katika tarafa hiyo.
"Nawaomba wakaazi wote kushirikiana na utawala wa tarafa hii ili tuweze kuimarisha usalama katika eneo hili ili viwango vya maendeleo viweze kuimarika," alihoji Koech.
Adha, alisema kuwa yeye kama mkuu wa tarafa hiyo ya Gesima anaunga mkono Machifu wote kwa msako wa pombe haramu wanaoendesha ili kuhakikisha kuwa biashara hiyo haramu yapombe umekoma.
Koech, aliwatahadharisha wanywaji pombe na wagema kuachana na biashara hiyo ya pombe haramu ambayo inaendelea kuwauwa watu katika pande zingine za Kenya ili nao wasije wakapatwa na mtego huo.
"Nawaunga mkono Machifu na Naibu wao na ninawaomba wasije wakalegeze kamba katika vita dhidi ya pombe haramu maanake nipo tayarii kushirikiana nao," aliongezea Koech.
Kwa upande wa wizi aliwaonya wote ambao wanatajwa kuwa wanahusika katika lokesheni zote za Mochenwa na Nyamakoroto huku akiwaonya kuwa wanastahili kujisalimisha kabla siku zao kufika.
Mkuu huyu alisema kuwa wakaazi wote wakishirikiana itakuwa njia moja ya kuinua viwango vya maendeleo katika tarafa hiyo na Wadi ya Gesima kwa jumla.