Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakazi wa eneo la Kivaa katika kaunti ndogo ya Masinga, Kaunti ya Machakos wana sababu ya kutabasamu, baada ya kampuni ya Kengen pamoja na maafisaa wa shirika la ukulima la PERI kuwapatia mbegu za kupanda aina ya Nduma ambayo inajulikana kufanya vizuri kwenye maeneo makavu.

Vilevile, naibu wa chifu eneo la Kaewa bwana Josphat Mawia aliwaonya wakulima watakaonufaika na mbegu hizo kutoziuza ila wazitumie vizuri na wahakikishe mazao yao ni mazuri pale mvua kubwa ya El Nino ambayo inatarajiwa itakapoanza.

"Watakaonufaika na mbegu hizi zitumieni vizuri ili ziwanufaishe, msiuze mbegu hizi kisha mbaki mkihangaika. Tumieni fursa hii vyema kwani mavuno mazuri faida kwenu," alisema Mawia.

Pia afisa huyo aliwahimiza wenyeji hao kuhakikisha wametayarisha mashamba yao na kupanda mapema ili kupata mazao mazuri.

Maeneo mengine yaliyonufaika na mbegu kutoka kwa kampuni hiyo ni kama Ndithini, Mavyurya, Mananja na mengineyo.