Wakazi wa wadi ya Gesima kaunti ya Kisii wameiomba serikali ya kaunti kuwapa vijana walioacha kunywa pombe ajira kama njia ya kuwazuia kujihusisha na uhalifu.
Wakizungumza na wanahabari siku ya Jumatano katika wadi ya Gesima eneo bunge la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira, wakaazi hao wakiongozwa na Joseph Nyandega walisema wanahofia vijana hao wataanza kuwaibia mali yao.
"Pombe ilikuwa inawatuliza kidogo, wakati huu sasa hawana kazi na uzembe ni mwingi. Ni rahisi wao kuanzia kuiba kwani pia pombeiliyoko ni ghali," Nyandega alisema.
Hii ni baada ya ng’ombe mmoja kuibwa kutoka kwa mkazi mmoja katika wadi hiyo ya Gesima. Baadaye ng'ombe huyo alipatikana akiwa amefungwa wa kamba mpakani mwa shamba la mkazi huyo huku wengi wakisema huenda aliyemwiba ng’ombe huyo aliogopa na kumrudisha.
“Tunaomba serikali itafutie vijana hawa ajira hata kama ni ya kufagia masoko bora wasikae nyumbani. Wakikosa ajira wataanza kutuibia mali zetu hapa nyumbani,” Hellen Omwenga mkazi wa Gesima alisema.
Wakazi wengine hata hivyo walikuwa na mtazamo tofauti huku wakikashifu kitendo cha kuaribu mali wakati polisi walikuwa wakimwaga pombe haramu.