Share news tips with us here at Hivisasa

Waokongwe wa eneo la Masaba, Kaunti ya kisii wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kupokea fedha za wakongwe kutoka kwa serikali kuu.

Wakongwe hao walifurika mji wa Masimba siku ya Jumanne na ya Jumatano, huku wakiweka foleni ndefu wakitegea kupokea ufadhili huo ambao ulichukua siku mbili.

Akina mama wakongwe ndio walikuwa na idadi kubwa ya waliopokea pesa hizo katika eneo hilo la Masaba na Kaunti nzima ya Kisii. Hayo ni kwa mujibu wa afisi ya mipango maalumu ya serikali kuu tawi la Masaba.

"Tumefurahia sana kwa mara ya kwanza akina mama na wazee wakongwe kupata pesa hizi na tunaipongeza serikali kuu kwa kuleta mpango huu kwa wakongwe nchini," alisema Mwakilishi wa Wadi ya Gesusu bwana Samy Keronche aliyekua akiwaongoza wakongwe hao katika maeneo ya Masimba wakipokea pesa hizo.

Wakazi wa eneo hilo pia walifurahia sana kuwa serikali sasa imewajali wazee hao kwa kuwafidia ili pia wajikimu kimaisha na kuanzisha miradi ndogo ndogo.

"Naishukuru sana serikali maana pesa hizi tumekua tukisikia zipo, lakini eneo hili sasa ndio mara ya kwanza kuzipata kutoka kwa serikali kuu kupitia tawi la hapa Masaba na tunaiomba iendelee kuwajali wakongwe ili pia tujiendeleze kimaisha kwa kupata lishe na mahitji mengine ya kila siku bila kutegemea sana wasiokua karibu nasi," alisema Mama Agnes Mecha.

Mamia ya wakongwe hao walikita kambi katika maeneo hayo tangu siku ya Jumanne hadi Jumatano wakipokea pesa hizo.