Wakulima katika Kaunti ya Kisii wameonywa dhidi ya kununua mbolea bandia kutoka kwa baadhi ya wafanyibiashara.
Onyo hiyo imetolewa baada ya kuguduliwa kuwa baadhi ya wafanyibiashara huuza mbolea ambayo si halali na haijaidishwa na wizara ya kilimo huku msimu wa upanzi unapoendelea katika sehemu mbalimbali katika eneo la Gusii.
Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu mjini Kisii, afisa mkuu wa wizara ya kilimo katika kaunti ya Kisii Nathan Soile aliwatahadharisha wakulima kutonunua mbolea ambayo huuzwa katika masoko mbalimabali na kuwaomba kununa mbolea ya serikali kwa bei ya chini ili kuitumia kwa upanzi.
Kulingana naye, mbolea ambayo huuzwa kwa masoko, huwa zimefunguliwa na madini ambayo hupatika kwa mbolea huwa zimepotea.
Hii ni baada ya wafanyibiashara kupatikana wakiuza mbolea ambayo haijaidhinishwa na Wizara ya Kilimo katika eneo la Suneka na Daraja mbili.
“Mbolea hiyo ambayo inauzwa kwa masoko ni mbaya kwa mimea. Wakulima wanapaswa kuenda kwa duka zile zimeidishwa kuuza mbolea ikiwa wanataka mazao yao yafanye vyema shambani,” alisema Soile.
Aliongezea, “Nawahimiza wakullima wanunune mbolea kutoka kwa duka ambazo zimeidhinishwa na wazara ya kilimo.”