Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakulima kutoka Kaunti za Nyamira na Kisii wameshauriwa kuanza kilimo cha mmea wa 'macadami.

Akizungumza siku ya Jumatano, anayesimamia idara ya kilimo katika Kaunti ya Kisii Vincent Sawe, alisema kuwa kuna hitaji kubwa sana ya 'macademia' katika masoko ya humu nchini na baadhi ya nchi za Afrika.

Alisema kuwa zao hilo ambalo matunda yake huwa na mwonjo kama wa njugu, huuzwa kwa shilingi mia moja kila kilo hivyo huwa na faida kubwa kwa mkulima yeyote ambaye anafanya kilimo hicho.

Sawe pia aliwasihi wakulima kujaribu kupanda aina nyingine za mimea ili kuboresha na kuimarisha usambazaji wa chakula na uwepo wa chakula cha kutosha kwenye nyumba na nchi kwa jumla.

"Kaunti yetu ya Kisii imekuwa yenye rotuba. Wakulima tunapaswa kutumia udongo wetu kwa manufaa yetu na tuwe tukipanda aina nyingi za mimea. Tukifanya hivyo tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwa na vyakula tele na vingine mtauzia walio na hitaji la chakula si tu hapa bali Kenya nzima," alisema Sawe.

Aidha, aliwashauri wakulima kutembelea taasisi ya mafunzo ya wakulima ilioko mjini Kisii kupata ushauri na maelekezo ya jinsi ya kuboresha kilimo hicho cha 'macadamia' na ukulima mwingine wa mimea mipya katika nyanja za kilimo kama njia mojawapo ya kujiendeleza kimapato.