Walemavu ambao wako katika mitaa mbalimbali mjini Kisii wameshauriwa kuondoka mara moja.
Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa walemavu hao huja mitaani kuombaomba pesa. Serikali ya kaunti ya Kisii yasema tayari imepanga jinsi ya kuwasaidia walemavu hao.
Akiongea Jumatatu mjini Kisii, rais wa walemavu katika kaunti ya Kisii Kombo Mouko alisema kuwa serikali ya kaunti imesema itawaangalia na kuwashugulikia kikamilifu baada ya serikali hiyo kutangaza kusajiriwa kwa walemavu vijijini ili kupokea usaidizi na kusema kwa sasa walemavu wanastahili kuondoka mitaani .
Kulingana na Mouko, walemavu wamekuwa wakienda masemina na kupokezwa mafunzo jinzi watakuwa wakiishi wakiwa na ulemavu.
“Naomba walemavu waondolewe kwa mitaa maana pesa zao zitawafikia hivi karibuni na ninaomba wale walemavu hawajasajiliwa wajaribu wasajiliwe kwa serikali ya kaunti ili wasaidiwe,” alisema Mouko.
“Kuomba omba pesa kwa wapiti njia si suluhisho hata yule humpokeza mlemavu pesa huchoka akiwa anakupata anamuomba kila. Naomba walemavu hao wawaondoke katika mji huu wa Kisii,” aliongeza Mouko.
Pia Mouko alikiri kuwa walemavu wengine ni wananchi wa nchi jirani ya Tanzania. Alisema waondolewe na warudishwe nchini mwao ili wapate misaada katika nchi yao.