Share news tips with us here at Hivisasa

Waliosomemea taaluma ya udaktari na ualimu katika Kaunti ya Kisii na hawajapata ajira wana kila sababu ya kutabasamu baada kupata ujumbe kuwa watapata ajira nchini Angola.

Akizungumza mnamo siku ya Alhamisi katika mji wa Kisii, mwenyekiti wa bodi ya kuwaajiri wafanyikazi katika kaunti hiyo Bw David Kombo alisema wanaotoka Kaunti ya Kisii waliosomea taaluma hizo mbili na hawajapata ajira nchini wataajiriwa katika nchi ya Angola.

Ujumbe huo ulitolewa baada ya Balozi wa nchi ya Angola nchini Kenya Virgílio Marques de Faria kutembelea Kaunti ya Kisii sikuya Alhamisi na kusema nchi ya Angola ina ushirikiano mwema na nchi ya Kenya, jambo ambalo litalipelekea taifa hilo la Angola kuwaajiri baadhi ya walimu na madaktari kutoka nchini Kenya ambao hawajapata nafasi ya kuajiriwa.

“Zile changamoto ambozo vijana wa nchi ya Kenya wanazipitia haswa kutopata ajira baada ya masomo huenda zifike mwisho kupitia ajira nchi ya Angola inapania kuwapa baadhi ya wale waliosomea udaktari na ualimu,” alisema Virgílio, balozi wa Angola humu nchini.

Wakati uo huo, mwenyekiti Kombo alifurahishwa na hilo na kuweka maelewano hayo na serikali ya Kaunti ya Kisii huku akimwakilisha Gavana wa kaunti ya hiyo James Ongwae ambaye hangeweza kufika katika kikao hicho.

Balozi wa Kenya nchini Angola Josephat Maikara naye pia alihudhuria kikao hicho na kuweka maelewano hayo pamoja.