Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanaoishi karibu na barabara katika Kaunti Ndogo ya Muhoroni watahitajika kuzingatia sheria za Wizara ya Ujenzi na Barabara na zile za Kampuni ya umeme nchini, Kenya Power wanapopanda miti kando ya barabara.

Hili linajiri wakati ambapo wakazi waliopanda miti karibu na nguzo ya nguvi ya umeme kupata hasara wakati miti yao ilipoangushwa na kampuni hiyo ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea wakati miti hiyo inapokuwa refu na kuhitilafiana na nyaya za umeme.

Hali hiyo inawakumbusha wakazi taswira ambapo majanga mengi ambayo yamewahi kutokea nchini yakisababishwa na miti inayopandwa karibu na maeneo yaliyopitishwa umeme.

Miti hiyo inapokuwa mikubwa hutingika hasaa nyakati za upepo mkali na mvua hali inayosababisha nyaya za umeme kuguzana na hapo kusababisha mlipuko wa nguvu za umeme.

Wakati mwingine hali huwa mbaya zaidi wakati miti hiyo inapoangukia nyaya za umeme. Hapa mengi yatastahili kufanyika ikiwemo kuhamasisha umma kuhusu namna ya kupanda chochote wala kuweka mijengo kando ya barabara, ikizingatiwa kuwa wakati mwingine wananchi wanaoishi karibu na barabara hulazimika kuhama na hata kupata hasara wakati mali yao inapoharibiwa kufutia ubomozi wa vitu kama vile nyumba.