Wanaume wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kujua hali zao za ugonjwa wa saratani ya matiti kwani wako katika nafasi kubwa ya kupata ugonjwa huo.
Akizungumza siku ya Jumamosi katika hospitali ya Aghakhan wakati wa uchunguzi wa bure wa saratani ya matiti, daktari wa saratani ya matiti Ronald Wamalwa aliwataka wanaume kutoa dhana kuwa ugonjwa huo huwa wa wanawake pekee.
Aidha, Profesa Wamalwa alisema kuwa wanaume wengi ufura matiti kinyume na maumbile, ishara tosha kuwa hili ni thibitisho mojawapo wa dalili ya saratani.
Vile vile, aliongeza kuwa kaunti ya Mombasa ni mojawapo ya maeneo yanayoripotiwa kuwa na wanawake walio na saratani ya matiti kupitia urithi.
Aliongeza kuwa baadhi ya dalili za maradhi hayo amesema ni kufura ndani ya titi bila maumivu, kutoa damu ama usaha na pia kuanza kutoa maziwa kabla ya wakati wake.
Wakati huo huo, Fridah Odondi muathiriwa wa saratani wa miaka mingi aliwashauri wanawake na wanaume kutopuuza hali zao na pia kukubali matibabu kwani yeye pia alikatwa matiti yake yote mawili na anaishi vyema.