Share news tips with us here at Hivisasa

Maafisa wa polisi wa kituo cha Keroka, Kaunti ya Nyamira wamewatia mbaroni washukiwa wawili wa mauaji ambao wanashukiwa kumuua ajuza wa miaka 72 majuma mawili yaliyopita.

Ajuza huyo, Teresa Manyara kutoka kijiji cha Bochari, aliuawa na washukiwa wa ujambazi nyumbani mwake.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu afisa mkuu wa kitengo cha ujasusi wilayani Masaba kaskazini Irene Agola alisema waliwatia mbaroni washukiwa hao baada ya kufanya uchunguzi wao wa kina na wanaendelea kutoa usaidizi zaidi kwa maafisa hao wa polisi.

Washukiwa waliotekeleza mauaji hayo walitoa mabati kwenye paa la nyumba ya ajuza huyo na kuingia ndani na kumuitisha pesa. Aliposema kuwa hakuwa na pesa, majambazi hao walimpiga ajuza huyo hadi kufa.

Washukiwa hao wanazuiliwa katika kituo cha Keroka wakiendelea kutoa usaidizi kwa uchungunzi.

“Tumewatia mbaroni washukiwa hawa wawili wa mauaji na wanaendelea kutusaidia kwa uchunguzi zaidi kisha baadaye watakabiliawa kisheria,” alisema Agola.