Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wazazi katika kaunti ya Kisii wameshauriwa kukaa na watoto wao nyumbani mgomo wa walimu unapoendela kushika kasi kote nchini.

Wito huo umetolewa baada ya baadhi ya wanafunzi wa shule za upili kuenda shuleni kujisomea jambo ambalo limeshukiwa kuwa hatari kwani huenda baadhi yao wajihusishe na masuala ya mapenzi na kuwapelekea wengi kupata magonjwa yazinaa huku wengine wakipata mimba.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu mjini Kisii wakati wa maandamano ya walimu wa chama cha Kuppet na Knut naibu katibu wa chama cha Knut tawi la Kisii kusini Victor Ombasa alisema ikiwa wazazi wanahitaji watoto wao kuwa katika hali salama wakae na watoto wao nyumbani.

“Kuna uwezekano wa wanafunzi kujulisha wazazi wao kuwa wanaenda shuleni kujifunza au kujisomea na baadaye wanajihusisha kwa visa vya mapenzi amabavyo vitawawezesha kupata magonjwa na kupelekea kupata mimba,” alisema Ombasa.

Aliongezea ”Ushauri wangu kwa wazazi ni kuwa wazazi wakae na watoto wao nyumbani hadi walimu warejee shuleni baada ya kupokezwa nyongeza ya mishahara yao.”

Aidha, katibu huyo alisema hawatakubali vyovyote kuwa na mazungumzo na serikali hadi waongezewe pesa zao.

“Walimu tumechoka zaidi na hatutarudi shuleni hadi tupate nyongeza ya mishahara. Watoto waendelee kusalia nyumbani,” alisema Ombasa.