Wazee kutoka katika jamii ya Wakalenjin chini ya muungano wa 'Kalenjin Global Welfare Society' wametaka msiruru ya maombi kwa naibu rais William Ruto na mwana habari Joshua Sang Kusitishwa.
Waiongozwa na askofu Cornelius Korir, walisema maombi hayo yameanza kuchukua mkondo ambao unaweza ukayumbishwa umoja wa Wakenya.
Korir alitaka viongozi wa kidini ambao wamekuwa wakiongoza maombi husika kuendeleza maombi kwa wawili hao katika makanisa yao badala ya kuzunguka kote nchini kwa madai ya kuwaombea wawili hao.
“Kile nimesema tangu mwanzo, maombi haya si mbaya lakini yafanyiwe kanisani ili kuzuia wanasaisa kutumia nafasi hiyo kutoa matamshi ya kucochea Wakenya,” alisema askofu Korir.
Akihutubu baada ya kukutana na wazee kutoka katika jamii hiyo katika dayosisi ya kanisa la katolikli mjini Elodret, askofu Korir alisema matamshi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakishiriki katika maombi hayo yameanza kuchochea uhasama miongoni mwa Wakenya.
Msimamo wa askofu Korir uliungwa mkono na mwenyekiti wa muungnao wa wazee hao Simon Markelda, ambaye alisema wakati umefika kwa wanasiasa kuacha kutumia masaibu ya Ruto na Sang kujiptia umaarufu.
“Sisi kama wazee tunajua Mungu husikia maombi lakini si maombi ya kuzunguka kote nchini na wanasiasa wale ambao hata wengine wao hawajui Mungu,” alisema Mzee Markelda.
Mbali na mombi hayo, askofu Korir alikosoa wanasaisa ambao wameanza kusema wana ushahidi kuhusu watu ambao walipanga njama ya kumhusisha Ruto na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/2008.
Askofu Korir alitaka wale watu ambao wana ushahidi kuhusiana na kesi hiyo kuwasilisha ushahidi wao katika mahakama ya ICC, badala ya kutoa matamshi ambayo yanaweza yakachoche Wakenya.
Matamshi ya askofu Korir yamewadai siku chache baada ya mkutano wa maombi kwa wahasiriwa ambao ulikuwa umepangwa kufanyika mjini Eldoret kuhairishwa.