Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Nyali Hezron Awiti amewataka polisi kuandamana kutetea haki zao pindi tu mmoja wao anapouliwa na wahalifu.

Akiongea siku ya Jumanne kwenye maadhimisho ya siku kuu ya Mashujaa katika uwanja wa michezo wa Mombasa, Awiti aliwakashifu viongozi wa mashrikia ya kutetea haki za binadamu kwa kutojali na kutetea polisi wanapovamiwa na kuuaawa wakati wa uahalifu.

Awaiti aliwataja polisi kama binadamu wa kawaida na wanahitaji utetezi wakati wanapokabiliwa na matatizo.

Aidha, amewataka wananchi kushirikiana na polisi ili kupunguza visa vya ukosefu wa usalama jijini Mombasa, ambavyo vimekua vikiongezeka kila kuchao.

Kauli yake inajiri kutokana na kuongezeka kushuhudiwa visa vya kuuawa kwa polisi jijini Mombasa, kisa cha hivi karibuni kikiwa ni kuawa kwa afisa mmoja aliyepigwa risasi eneo la Bondeni na watu wasiojulikana.