Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Chifu wa lokesheni ya Mwamonari, eneo bunge la kitutu Titus Mochiemo amewaomba watu wote wa lokesheni hiyo kuhudhuria vikao vya mabaraza pindi vinapoandaliwa, ili kupashwa yale yanayoendelea.

Hii ni baada ya watu wachache kuhudhuria kikao cha baraza kilichoandaliwa katika eneo la Getunwa siku ya Jumanne, jambo ambalo halikumfurahisha chifu huyo.

Akiongea katika baraza hilo, Mochiemo aliomba watu kuheshimu yale wanapashwa kupitia wazee wa vijjiji, na kuhudhuria vikao hivyo kwani ni mengi huwa yanazungumziwa hasa yale yatawasaidia na kujua jinsi mambo yanavyoendeshwa kwa lokesheni.

“Naomba kila mtu ambaye ako kwa lokesheni hii yangu awe anahudhuria mabaraza maana kuna jambo linaniwezesha niandae kikao ili niwape habari ya lokesheni yangu,” alisema Mochiemo.

“Kwanzia leo naomba kila mtu ajulishwe habari hii ya kuhudhuria mabaraza kwani kuna mambo ya kiusalama yanazungumziwa, wizi, ujambazi na mengine mengi lakini ukikaa kwa nyumba huwezi jua lile tunaliongea,” aliongeza Chifu.

Vilevile, wazee wa kijiji ambao walikuwa kwa baraza hilo hawakufurahishwa na watu wachache walioudhuria.

“Tunaenda kupitisha sheria kwa wale hawakuji kwa mabaraza ili wakabiliwe kisheria, hatuwezi fanya kazi ya bure kwa kuwafahamisha watu kuhudhuria mabaraza katika vijiji vyetu na wanakosa kufanya hivyo,” alisema Cleophas Ondimu, mzee wa kijiji cha Biyoki.