Chifu wa lokesheni ya Mochenwa amesema orodha ya majina ya wagema imesaidia kupunguza pombe haramu katika eneo hilo.
Chifu huyo alisema lita zaidi ya mia moja za changaa na lita hamsini za busaa zimemwagwa katika eneo hilo.
Akiongea siku ya Jumanne katika ofisi yake, Chifu Magara Makori alisema kuwa orodha hiyo ambayo iliotolewa na wanainchi kwa manaibu kwa ushirikiano wa wazee wa vijiji imesaidia pakubwa kupunguza pombe haramu katika lokesheni hiyo.
Magara aliongezea kuwa orodha hiyo imesaidia pakubwa kwani waliweza kuenda kwa nyumba za wagema waliotajwa na kufanya msako mkali ili kuhakikisha kuwa uzaji wa pombe haramu umeisha katika lokesheni hiyo.
Aidha, alisema kuwa siku ya Jumapili na Jumatatu walimwaga zaidi ya lita mia moja za changaa na lita hamsini ya busaa huku akiahidi kuendela na vita didhi ya pombe haramu katika eneo hilo.
“Nimeona kuwa watu wanaendelea kujiepiusha na kutengeneza pombe haramu katika lokesheni hii. Bado nitaendelea kupambana na wale wagema wachache amabo wametia maskio yao nta,” alisema Chifu Magara.
Chifu huyo alisema kuwa huu ni wakati wa kufanya maendeleo kwa kuwa serikali ya kaunti inatoa pesa za kuazisha miradi mbalimbali kwa watu waliojiunga katika vikundi vya maendelo na kuasi pombe haramu.