Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Huku maeneo mengi katika kaunti takribani zote kutoka eneo la pwani yakishuhudia uhaba wa maji, Chuo Kikuu cha Pwani kimefungwa kwa muda usiojulikana kwa madai ya kukosekana kwa maji ya kutumiwa.

Kulingana na chansela mkuu wa chuo hicho ambaye aliongea na waandishi wa habari siku ya Jumatano, siku moja baada na kufungwa kwa chuo hicho, Profesa Mohamed Rajab alisema kuwa walichukua hatu hiyo baada ya maji ambayo walikuwa wanatumia chuoni humo kuisha na ikabidi usiumamizi wa chuo kuamua hivyo.

Profesa Rajab alidai kuwa maji ambayo walikuwa wanatumia yalikuwa ya kisima cha shule, na tayari yalikuwa yameisha, na hivyo basi ikawa vigumu kwa shughuli za kawaida kuendelea chuoni ikizingatiwa kuwa wanafunzi pamoja na wahudumu wa chuo hutumia maji kwenye shughuli za kila siku.

“Chuo kilitumia maji ambayo yalikuwamo yakaisha na hakukuwa na njia nyingine ya kupata maji kwa sababu yale ya kampuni yalikatwa, na shughuli haziwezi kuendelea bila maji,” alisema Rajjab.

Kulingana na taarifa kutoka kwa kitengo cha kampuni ya kusimamia huduma za maji ya COWAS, hatua ya kukatiza huduma za maji kwenye mashirika ya kusambaza bidhaa hiyo ni kuwapo kwa deni la jumla la takribani bilioni 1.2, ambazo zinadaiwa kaunti tatu za eneo la pwani.

Hatua hiyo imeshuhudia milolongo ya wakazi wakiwa katika maeneo ya mifereji ya visima vya watu binafsi wakisaka bidhaa hiyo angalau kukithi mahitaji ya nyumbani.