Wakaazi katika kaunti ya Nyamira wamempongeza Gavana wa kaunti hiyo John Nyagarama kwa kufadhili wanafunzi wa shule ya wavulana ya Nyamira godoro, blanketi na vipande vya sabuni baada ya shule hiyo kuchomeka.
Hii ni baada ya bweni ya wanafunzi wa shule hiyo ya wavulana ya Nyamira kuchomeka siku ya Jumanne mwendo na kusababisha mali ya thamani yasiojulikana kuaribika katika shule hiyo.
Wakiongea na waandishi wa habari siku ya Jumatano katika uwanja wa shule hiyo ya Nyamira wakati Gavana John Nyagarama alikuwea anafadhili wanafunzi hao bidhaa hizo, walimpongeza gavana kwa ufadhili huo.
“Mimi ni mzazi wa mwanafunzi anayesoma katika shule hii katika kidato cha nne. Sikuwa na pesa za kununua ingine lakini gavana amefanya vizuri na ninamhukuru sana. Namuomba aendelee na usaidizi wa aina hiyo," alisema Cecilia Kerubo, mzazi.
“Tumefurahishwa na jambo ambalo gavana wetu amefanya la kuwanunulia wanafunzi ambao walipoteza vitu vyao kupitia mkasa wa moto godoro na blanketi. Huo ndio uongonzi tunaohitaji hapa Nyamira,” alisema Victor Osano, mkazi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Jelard Orina alisema chanzo cha moto huo hakijabainika lakini uchunguzi ungali unaendelea.
Kwa upande wake Gavana John Nyagarama alisema tayari serikali yake imetenga shillingi million 30 ambazo zitanunua gari za kuzima moto ambazo zitasaidia pakubwa mikasa ya aina hiyo inapotekokea.