Mwenyekiti wa vyuo vya ufundi eneo bunge la Bochari, kaunti ya Kisii, James Nyamweya Kiyondi, ameomba gavana wa kaunti hiyo James Ongwae kuajiri walimu wengine katika vyuo hivyo.
Akiongea na wanahabari siku ya Alhamisi ofisini mwake, alisema kuna uhaba wa walimu wa kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo hivyo na kuomba gavana James Ongwae kuongeza walimu ili wanafunzi wawe wakipata mafunzo kikamilifu ili waje kujisaidia nyakati za usoni.
“Nashukuru serikali ya kaunti ya Kisii kwa yale imetekeleza kwa vyuo vya ufundi za kaunti hii. Naomba waendelee na usaidizi ili viwango vya elimu viinuke zaidi katika kaunti hii haswa katika vyuo vya ufundi,” Nyamweya.
“Kuna uhaba wa walimu katika vyuo hivi vya ufundi na naomba serikali ya kaunti ya Kisii kupitia gavana wetu, iajiri walimu wengi ili wanafunzi wapate masomo ya kiwango cha kutosha,”aliongeza Nyamweya.
Wakati huo huo, mwenyekiti huyo alisema kwanzia mwaka huu, wanafunzi wote wa kaunti ya Kisii watakuwa wakifanyia mitihani yao katika chuo cha kiufundi kilichiko katika kaunti hiyo. Hapo mbeleni walikuwa wakienda hadi mjini Kisumu kufanya mitihani lakini kwa sasa watakuwa wakifanyia katika Kaunti ya Kisii.
“Naomba wazazi kuwaleta watoto wao ili wajiunge na vyuo hivi waweze kupata elimu ambayo itawasaidia nyakati zijazo,” alisema Nyamweya.